Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Chaipinga TCU.Chasema Hakijawahi Dahili Wanafunzi Vilaza
Siku moja baada ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kutangaza utata wa udahili wa wanafunzi wa vyuo vikuu, wadau wakubwa wa elimu, wamejitokeza kupinga hatua hiyo. Wadau hao ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) .
UDSM kimeeleza kwamba hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyedahiliwa chuoni hapo, ambaye hana sifa za kujiunga na chuo hicho.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Florens Luoga alisema
jana kuwa chuo hicho kimeweka utaratibu ambao unaweza mwanafunzi yeyote
anayedahiliwa chuoni hapo, awe na sifa zinazohitajika kwa kuwa
hawafanyi biashara.
“Sisi
hapa ni wakali kuhusu jambo hilo, tukibaini kuwepo kwa mwanafunzi
ambaye hana sifa tunamfukuza. Hatusubiri TCU iseme...hata tukibaini kuwa
mtu alifanya udanganyifu na alishamaliza chuo, lakini hakuwa na sifa,
tunamnyang’anya digrii tuliyompa,” alisema Profesa Luoga na kuongeza:
“Hiki
ni chuo, hatufanyi biashara, sisi kazi yetu hapa ni kuandaa wataalamu
na ndio maana tunakuwa wakali na makini kuhakikisha wanafunzi
tunaowachukua, wote wanakuwa na sifa stahiki”, alisema
Profesa Luoga alisema uhakiki ambao umefanywa na TCU na kutoa idadi ya wanafunzi 224 wanaosoma chuoni hapo, kuhakikisha wanawasilisha ushahidi wa nyaraka zao, wanaufanyia kazi, kwani kuna uwezekano tume hiyo haina taarifa kuhusu programu zinazoendeshwa na chuo hicho.
Profesa Luoga alisema uhakiki ambao umefanywa na TCU na kutoa idadi ya wanafunzi 224 wanaosoma chuoni hapo, kuhakikisha wanawasilisha ushahidi wa nyaraka zao, wanaufanyia kazi, kwani kuna uwezekano tume hiyo haina taarifa kuhusu programu zinazoendeshwa na chuo hicho.
Alifafanua
kuwa kuna baadhi ya programu maalumu, ambazo Serikali ya Tanzania
imeingia na nchi nyingine kwa ajili ya kuendesha programu maalum.
Alisema
kozi hizo zimekuwepo chuoni hapo kwa muda wa miaka 40 sasa na
zinafanywa kutokana na makubalino ya Serikali ya Tanzania na nchi
husika.
Alisema
chuo hicho kikongwe Tanzania, kutokana na kuwepo makubaliano hayo
kimekuwa kinapokea baadhi ya wanafunzi ambao wanatoka nje ya nchi na
akasisitiza kuwa yawezekana ndio hao ambao TCU imeshindwa kupata nyaraka
zao.
“Yawezekana kuna taarifa ambazo hazijakaa sawa, tumepokea taarifa ya TCU sisi kama chuo ni jukumu letu kuitekeleza,” alieleza Profesa Luoga.
Comments
Post a Comment