TRA yaidai ACACIA trilion 425 kwa ukwepaji kodi tangu maka 2000
Kampuni
ya Acacia imeeleza kuwa imepokea taarifa kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) inayoonyesha kuwa migodi yake ya Bulyanhulu inadaiwa kodi
ya kati ya mwaka 2000 hadi 2017 na Pangea inadaiwa kodi ya kati ya
2007-2017.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya Acacia jana Julai 24,
imeeleza kuwa taarifa hiyo imetokana na ripoti za kamati mbili za Rais
zilizoonyesha kuwa wamekuwa hawatangazi kiasi halisi cha mapato yao
wakisafirisha mchanga kwenda nje ya nchi.
Acacia
wamesema kuwa, bado wanaendelea na msimamo wao wa kupinga matokeo ya
kamati hizo na kusema kuwa wamekuwa wakitangaza mapato yao.
Aidha,
wameeleza kwamba bado hawajapata nakala za ripoti za kamati ya kwanza
na ya pili zilizowasilishwa kwa Rais Magufuli Mei 24 na Juni 12 mwaka
huu.
Uchambuzi
uliofanywa na TRA umeonyesha kuwa Mgodi wa Bulyanhulu unadaiwa na
serikali takribani Tsh 344.8 trilioni (USD 154bn) na Mgodi wa Pangea
takribani Tsh 76.1 trilioni (USD 36bn).
Uchambuzi
huo unaonyesha kuwa Acacia wanadaiwa takribani Tsh 89.5 trilioni (USD
40bn), ikiwa ni malimbikizo ya kodi na Tsh 335.9 trilioni (USD 150bn)
ikiwa ni adhabu na riba.
Aidha, Acacia wamepinga uchambuzi huo, na kusema kuwa wanaufanyia kazi ili waweze kutoa maamuzi sahihi.
Comments
Post a Comment