Posts

WAZIRI SIMBACHAWENE APIGA MARUFUKU POLISI KUKAMATA WANANCHI, BODABODA BILA KUFUATA UTARATIBU, AAGIZA KILA OPERESHENI MKUU WA WILAYA APEWE TAARIFA, ASISITIZA UCHAGUZI MKUU WA HURU NA HAKI 2020

Image
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza katika Kikoa cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, wakati alipofika Wilayani humo kwa ziara ya kikazi. Simbachawene amepiga marufuku ukamataji wa wananchi, bodaboda pamoja na kufanya operesheni ya aina yoyote kwa kukurupuka bila kufuata utaratibu, hali inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani badala ya kujenga amani.. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza katika Kikoa cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mpwapwa, wakati alipofika Wilayani humo kwa ziara ya kikazi. Simbachawene amepiga marufuku ukamataji wa wananchi, bodaboda pamoja na kufanya operesheni ya aina yoyote kwa kukurupuka bila kufuata utaratibu, hali inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani badala ya kujenga amani. Watatu kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Jabir Shekimweri. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

MAKAMU WA RAIS SAMIA AHAKIKI TAARIFA ZAKE ZA MPIGA KURA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihakiki taarifa zake za mpiga kura kwenye Daftari la Wapiga kura katika Kituo cha Shule ya Sekondari  SOS Wilaya ya Magharibi (B) Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo Febuari 27,2020. katikati ni Mkurugenzi wa tume ya Uchaguzi Zanzibar  ZEC Thabit Idarous Faina.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionesha Kitambulisho Kipya cha Mzanzibari Mkaazi baada kukabidhiwa kitambulisho hicho na Afisa wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Jamii Zanzibar Khatib Said Bakari  leo Febuari 27,2020 Tunguu Zanzibar.    (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  

TRA yaidai ACACIA trilion 425 kwa ukwepaji kodi tangu maka 2000

Image
Kampuni ya Acacia imeeleza kuwa imepokea taarifa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inayoonyesha kuwa migodi yake ya Bulyanhulu inadaiwa kodi ya kati ya mwaka 2000 hadi 2017 na Pangea inadaiwa kodi ya kati ya 2007-2017. Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya Acacia jana Julai 24, imeeleza kuwa taarifa hiyo imetokana na ripoti za kamati mbili za Rais zilizoonyesha kuwa wamekuwa hawatangazi kiasi halisi cha mapato yao wakisafirisha mchanga kwenda nje ya nchi. Acacia wamesema kuwa, bado wanaendelea na msimamo wao wa kupinga matokeo ya kamati hizo na kusema kuwa wamekuwa wakitangaza mapato yao.  Aidha, wameeleza kwamba bado hawajapata nakala za ripoti za kamati ya kwanza na ya pili zilizowasilishwa kwa Rais Magufuli Mei 24 na Juni 12 mwaka huu. Uchambuzi uliofanywa na TRA umeonyesha kuwa Mgodi wa Bulyanhulu unadaiwa na serikali takribani Tsh 344.8 trilioni (USD 154bn) na Mgodi wa Pangea takribani Tsh 76.1 trilioni (USD 36bn).

Acacia wakutana na Rais Magufuli Ikulu leo, wakubali kulipa fedha wanazodaiwa..

Image
      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton na kukubaliana kuwa kampuni hiyo ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake hapa nchini. Prof. John L. Thornton ambaye amesafiri kwa ndege binafsi kutoka nchini Canada hadi Tanzania amekutana na Mhe. Rais Magufuli leo Juni 14, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam na mazungumzo yao yamehudhuriwa na Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Ian Myles na Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi. Baada ya Mazungumzo hayo Prof. John L. Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na pia ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa k

INASIKITISHA:SABA WAFARIKI KWA KUSOMBWA NA MAJI YA MVUA

Image
Jeshi la Polisi mkoani hapa limewataka wananchi kuwa makini na kuchukua tahadhari zote katika kipindi hiki cha Masika. Akizungumza na waandishi wa habari mchana wa leo ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna Charles Omari Mkumbo alisema katika kipindi hiki cha mvua wananchi hawatakiwi kuvuka mito na mabonde yenye maji kwa hisia badala yake wanatakiwa wawe na subira. “Natoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Arusha katika kipindi hiki cha masika hamtakiwi kujipa ujasiri na kuyakadiria maji ya mvua hivyo zinahitajika tahadhari za kutosha dhidi ya watoto, au vyombo vyovyote vya usafiri  kwani maji hayo huwa yanakwenda kwa kasi, yasubirini yapite acheni hisia ili kuhakikisha maisha yenu hayahatarishwi na mvua”. Alisisitiza Kamanda Mkumbo. Kamanda Mkumbo alitoa wito huo baada ya jana usiku kunyesha mvua kubwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huu na kusababisha vifo vya watu saba. Alisema katika tukio la kwanza jana Usiku wa saa 4:00 katika kijiji

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA RAIS WA IVORY COAST MHE. ALASSANE QUATTARA JIJINI ABIDJAN

Image
 Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu  Dkt. Jakaya Kikwete akikaribishwa na Rais Alassane Ouatara wa Ivory Coast jijini Abidjan katika Ikulu ya nchi hiyo. Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akimkabidhi ripoti ya 'Kizazi cha Elimu' Rais Allasane Ouatarra wa Ivory Coast  Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mazungumzo na Rais Alassane Ouattara. Kulia kwake ni Makamu wa Rais wa nchi hiyo Mhe. Daniel Kablan Duncan  Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiagana na Rais Alassane Ouattara baada ya mazungumzo yao   Ikulu ya Ivory Coast.  Rais MStaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Uongozi wa Watanzania wanaofanya kazi Benki ya Maendeleo ya Afrika jijini Abidjan  Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akifurahia mazungumzo na baadhi ya watoto wa Watanzania waishio Ivory Coast waliomtembelea hotelini kwake Abidjan Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiwasainia aut

Simba na Yanga zioneshe ukongwe wao uwanjani

Image
PAMBANO la watani wa jadi katika soka la Tanzania la Simba na Yanga linafanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Hilo ni pambano la marudiano baada ya lile la raundi ya kwanza kumalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 na baadhi ya mashabiki wa Simba kuleta vurugu kwa kuvunja viti vya uwanjani humo pamoja na vitu vingine. Uwanja huo ni wakisasa na wathamani kubwa na umejengwa kwa kodi za wananchi, hivyo kuharibu miundo mbinu yake ni kutowatendea haki Watanzania, ambao wengi wao ni wale wa kipato cha chini. Ni matarajio yetu kuwa, baada ya maandalizi ya muda mrefu ya timu hizo kwa ajili ya pambano hilo, bila shaka mchezo utakuwa mzuri utakaowafanya mashabiki kufaidi fedha zao walizotoa kwa ajili ya viingilio. Na uzuri wa mchezo wa soka sio timu kucheza vizuri, bali pia waamuzi kuchezesha kwa haki kwa kutumia sheria 17 za soka, mashabiki kuwa watulivu na mambo mengine kibao. Simba na Yanga ni timu kongwe kabisa hapa nchini, hivyo ni matarajio yet