INASIKITISHA:SABA WAFARIKI KWA KUSOMBWA NA MAJI YA MVUA
Jeshi la Polisi mkoani hapa limewataka wananchi kuwa makini na kuchukua tahadhari zote katika kipindi hiki cha Masika. Akizungumza na waandishi wa habari mchana wa leo ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna Charles Omari Mkumbo alisema katika kipindi hiki cha mvua wananchi hawatakiwi kuvuka mito na mabonde yenye maji kwa hisia badala yake wanatakiwa wawe na subira. “Natoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Arusha katika kipindi hiki cha masika hamtakiwi kujipa ujasiri na kuyakadiria maji ya mvua hivyo zinahitajika tahadhari za kutosha dhidi ya watoto, au vyombo vyovyote vya usafiri kwani maji hayo huwa yanakwenda kwa kasi, yasubirini yapite acheni hisia ili kuhakikisha maisha yenu hayahatarishwi na mvua”. Alisisitiza Kamanda Mkumbo. Kamanda Mkumbo alitoa wito huo baada ya jana usiku kunyesha mvua kubwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huu na kusababisha vifo vya watu saba. Alisema katika tukio la kwanza jana Usiku wa saa 4:00 katika kijiji